Mada Ya Pili

بِسْمِ اللهِ الَّرحْمنِ الَّرحِيْمِ

إنَّ اللهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِيْنُ Qur’an, 51: 58

وَكَأَيِّنْ مِنْ دَابَّةٍ لَا تَحْمِلُ رِزْقَهَا اللهُ يَرْزُقُهَا وَإِيَّاكُمْ وَهُوَ السَّمِيْعُ الْعَلِيْمُ Qur’an, 29: 60

Ewe muumini: Hakika umefahamu katika yale yaliyopita ni kiasi gani uadui na chuki unavyoacha madhara makubwa, basi tambua kwamba pupa ni ugonjwa vile vile kama magonjwa mengine, bali ni yenye madhara zaidi juu ya maisha ya kiislamu na ni mabaya juu yake.

Naam, pupa yenyewe ni sababu ya kukata tamaa na kukosa matumaini, tena ni ugonjwa na ni udhalili, na ndiyo sababu ya kunyimwa na uduni.

Hakika ushahidi wa wazi juu ya hii hukumu ya pupa, ni kile kilichowapata Mayahudi miongoni mwa udhalili na umasikini, na shida na uduni kwa ajili ya kupupia sana makapi ya dunia kuliko umma mwingine wowote.

Na pupa inadhihirisha athari yake mbaya kuanzia duara kubwa katika ulimwengu wa waliyo hai, na kuishia kwa kiumbe mdogo ndani yake, wakati kutafuta riziki ya tabu kwa kumtegemea Allah (s.w) inapelekea raha na utulivu na kudhihirisha athari yake yenye manufaa kila sehemu.

Mfano wa hilo: hakika mimea na miti yenye kuleta matunda inayohitaji riziki, -na ndiyo ambayo inazingatiwa kuwa katika viumbe hai,- hupelekewa riziki zake haraka ikiwa imetulia sehemu zake kwa kumtegemea Allah (s.w) na kukinai bila kudhihiri athari ya pupa, bali inawazidi wanyama kwa kuzaliana kwake na kulea matunda inayoyazaa.

Ama wanyama hawapati riziki zao isipokuwa baada ya juhudi kubwa na mashaka na kupata kiasi kidogo sana, hivyo ni kwa sababu wanataabika kwa pupa, na kuhangaika kutafuta riziki katika hali ya haraka.

Mpaka tunaona katika ulimwengu huo huo wa wanyama kwamba riziki hutolewa kwa watoto ambao wanaonesha kutegemea kwao kwa Allah (s.w) kwa lugha ya hali za udhaifu wao, na kutojiweza kwao, hupelekewa riziki yao iliyopangwa nzuri na iliyokamili kutoka katika hazina ya rehema ya Allah (s.w).

Wakati hawapati wanyama wakali ambao wanashambulia viwindwa vyao kwa pupa kubwa isipokuwa baada ya tabu na juhudi kubwa.

Basi hali hizi mbili zinabainisha kwa wazi kwamba: Pupa ni sababu ya kukosa, na tawakkuli na kanaa ni njia za rehema na wema.

Na tunaona hali hiyo hiyo katika ulimwengu wa mwanaadamu, kwani  Mayahudi ambao ni watu wenye pupa zaidi na maisha ya dunia, na wanayapenda maisha ya dunia kuliko ya akhera, bali wanayapenda pendo la ashki tena la uwendawazimu, mpaka wameyatangulia mataifa katika hili, hakika wamepigwa juu yao udhalili, na wakaelekezewa mashambulizi ya kuuliwa kwa mikono ya mataifa mengine.

Yote hayo kwa thamani ya kupata mali ya riba mbaya ya haramu baada ya taabu kwa muda mrefu, hawatoi humo isipokuwa kidogo sana, kana kwamba kazi yao ni kuihifadhi tu hiyo riba, basi inatubainishia hali hii: Kwamba pupa ni madini ya udhalili na hasara kwa binadamu.

Kuna matukio mengi yasiyohesabika kwamba mtu mwenye pupa daima, ni mwenye kuingia katika mkumbo wa hasara, mpaka imepita (Mwenye pupa ni mwenye kuharibikiwa, mwenye kula hasara) mapito ya methali zenye kuenea na wakaufanya watu wote kuwa ukweli wenye kuenea katika mtazamo wao. Basi maadamu jambo lipo hivyo, ukiwa unapenda mali sana basi itafute kwa kanaa bila ya pupa, mpaka itakujia kwa wingi.

Na inawezekana tukawafananisha wenye kukinai na wenye pupa ni kama watu wawili waingiao kwenye ukumbi wa dhifa kubwa aliyoiandaa mtu mkubwa mwenye cheo, anatamani mmoja wao kutoka ndani ya kina cha moyo wake kwa kusema: lau mkuu wa eneo angenipa makazi tu niokoke kutokana na baridi kali la nje ingenitosha, inanitosha hivyo. Na lau angeniruhusu kuketi kiti chochote katika sehemu ndogo, basi nayo ingekuwa ni fadhila kutoka kwake na ukarimu.

Ama mwingine anafanya kana kwamba ana haki juu ya wengine, kana kwamba wamelazimishwa wamsimamie kwa heshima na unyenyekevu. Hivyo anasema ndani ya kina cha moyo wake kwa udanganyifu: bwana mkubwa anatakiwa anipe kiti kikubwa na kizuri.

Na hivyo hivyo ndivyo anavyoingia ukumbini hali ya kuwa anabeba pupa hii, na kuziangalia sehemu tukufu katika viti. Isipokuwa bwana mkubwa mwenye ukumbi anamrudisha na kumueka katika sehemu ndogo, na yeye kwa upande wake anamkasirikia na kujaa kifua chake hasira juu ya bwana mkubwa.

Basi katika wakati aliotakiwa atangulize shukrani inayopasa yeye amefanya tofauti na yanayompasa, na kuanza kumkosoa, basi mwenye ukumbi akamuona mkorofi, akamkaribisha yule mtu wa kwanza ambaye aliingia ukumbini akiwa mnyenyekevu akitaka kukaa katika sehemu ya karibu iliyokuepo, kwa kuwa ilimfurahisha kanaa hii iliyodhihiri kutoka kwake, na ambayo imepelekea katika nafsi yake tukufu kufurahishwa na kupendezwa, na akawa anampa sehemu ya juu na nzuri na yeye kwa upande wake akazidisha shukrani zake, na radhi zake, na shukrani zake za dhati kila alipopanda vyeo.

Na hivi ndivyo ilivyo dunia, ukumbi wa wageni wa Rahman. Na uso wa ardhi ni meza ya rehema iliyotandikwa, na meza ya Rahman iliyoandaliwa, na daraja za riziki, na vyeo vya neema ni kama viti vya namna mbali mbali.

Hakika ubaya wa kuathiri kwa pupa, na ubaya wa mwisho wake kila mmoja anaweza kuuhisi, mpaka katika mambo madogo madogo.

Mfano: inawezekana kila mtu kuhisi huzuni na uzito moyoni mwake kwa ajili ya ombaomba anayemsisitiza kwa pupa kubwa, mpaka kwamba anamrudisha, wakati anahisi upole na huruma, kwa ajili ya ombaomba mwingine aliesimama kimya mwenye kanaa, na akatoa sadaka juu yake kiasi alichoweza.

Na mfano: Pindi utakapotaka kulala kidogo usiku ambao imekuwa shida kuupata usingizi, hakika utalala kidogo kidogo pindi utakapoupuuzia na kutoujali, lakini utakapoufanyia pupa na kukereka nao, na huku ukigalagala: ukijiuliza nitalala saa ngapi? Umeenda wapi usingizi? Ungepotea usingizi na kuukosa kabisa.

Na mfano: Unamsubiri mtu mmoja kwa kukosa subira, hali ya kuwa una pupa ya kukutana naye kwa ajili ya jambo muhimu, utahisi kero kwa kusema: Kwa nini haji, ana nini, mbona kachelewa? na mwishowe pupa inakuondoleaa subira na kukulazimisha kuacha mahala pa kusubiri kwa hali ya kukata tamaa. Na mara yule mtu uliyekuwa unamsubiri anakuja baada ya muda mchache, lakini kilichotarajiwa kinapotea na kuyeyuka.

Hakika siri iliyopo katika mfano wa matukio haya na hekima zake, ni: kama vile ambavyo upatikanaji mkate ni kwa kufuatana kazi za shambani za kupatikana ngano zisizokobolewa na kisagio, na jiko la kutengenezea mkate, vikifanyika mpangilio vitu hivi, hivyo hukutana na hekima ya kusubiri na kufanya mambo kwa pole pole.

Lakini mwenye pupa kwa sababu ya pupa yake hasubiri katika harakati zake wala hachungi viwango vilivyopo katika kupangika mambo, ima aruke na achupe na kudondoka, au aache moja ya viwango vilivyopangwa, basi vikiwa pungufu hafikii malengo yake aliyoyakusudia.

Enyi ndugu wenye kushangazwa na shida ya maisha, na wenye kuazimia kupupia dunia! vipi mnaridhia udhalili katika nafsi zenu kwa sababu ya pupa, – pamoja kwamba ndani yake kuna madhara haya na mabalaa,- na mnaziendea kila mali pasina kuangalia je, ni halali au haramu?

Na mnajitolea muhanga katika njia hiyo kwa mambo matukufu, na vitu vyenye thamani vinavyopaswa na maisha ya akhera, mpaka mnaacha nguzo muhimu katika nguzo za kiislamu kwa sababu ya pupa, nayo ni (Zaka) hali ya kutambua kwamba ni mlango adhimu unaomiminika kwayo baraka na utajiri kwa kila mtu, na kumuondoshea mabalaa na mitihani. Na wale wasiotekeleza zaka za mali zao bila shaka wanazikosa mali kwa kiwango chake, na kuzisambaza, ima katika mambo ya kipuuzi yasiyo na umuhimu nyuma yake, au kukumbwa na mitihani na kuwapokonya kabisa.

Na kwa hakika niliulizwa katika ndoto ya ajabu yenye ukweli, na hio ni katika mwaka wa tano wa vita vya kwanza ya dunia, na swali lenyewe ni:

 Ipi siri ya ulofa, na ufukara ambao umeupata umma wa kiislamu? na ni ipi siri ya uharibifu uliyozikuta mali zao na kuziharibu, na katika tabu na mashaka ambayo imedhoofishwa chini yake miili yao?

Hakika nilijibu swali hilo katika ndoto yangu ifuatavyo: Hakika Allah (s.w) ametufaradhishia katika kile alichoturuzuku katika mali zake (Al-ushr)

“Kutokana na mali zake Al-ushr” maana yake sehemu katika vifungu kumi, miongoni mwa vitu anavyovitoa, kama vile mimea. Mwandishi.

katika sehemu ya mali, na moja katika na arobaini

“Na moja kutokana na arobaini” maana yake kutokana na mali ya zamani (kama vile vitu na wanyama), ambayo Allah (s.w) mara nyingi huzalisha kutokana na hiyo mali katika kila mwaka ngamia kumi wapya. Mwandishi.

katika kifungu kingine ili atujaalie tupate thawabu za maombi ya kweli yanayofanywa na mafukara, na hutuepusha na mambo yanayochukiza nyoyoni mwao miongoni mwa chuki na hasadi. Isipokuwa sisi tumefunga mikono yetu kwa kuzipupia mali na hatukutoa zaka, na akairejesha Allah (s.w) zaka ile iliyo juu yetu kwa uwiano wa thelathini kati ya arobaini, na uwiano wa nane kati ya kumi.

Na akatutaka Allah (s.w) tufunge kwa ajili yake, na tupate njaa kwa ajili ya dini yake, njaa ambayo inakusanya faida na hekima zinazofikia faida sabini.

Ametutaka tuifanye katika mwezi mmoja katika kila mwaka, basi zikawa nzito katika nafsi zetu na kutuchukua huruma bila haki, na tukakataa kuvumilia njaa yenye kuburudisha ya muda mfupi, basi haikuwa kwa Allah (s.w), isipokuwa kutulipa aina ya swaumu na njaa yenye mitihani, ambayo inafikia mitihani sabini, na kutulazimisha juu yake muda wa miaka mitano mfululizo.

Na hivyo hivyo Allah (s.w) ametutaka tutekeleze aina za amri na maelekezo ya kiungu yaliyo mazuri yenye baraka ya hali ya juu, yenye nuru, tunazitekeleza katika saa moja kati ya masaa ishirini na nne.

Lakini tukafanya uvivu kuzitekeleza swala hizo, maombi, na nyiradi, tukaipoteza saa moja hiyo pamoja na saa nyingine.

Basi ikawa kutoka kwake (s.w) kutufutia madhambi kutokana na mabaya yetu na mapungufu, na akatufanya tulazimike kutekeleza aina ya ibada na swala kwa kutamkisha maelekezo na mafundisho, na kurudi na kukimbia na kuchupa na kushambulia na jambo linalofanana na haya, katika muda wa miaka mitano mfululizo.

Naam, hivi ndivyo nilivyosema katika ndoto ile, kisha nikazindukana, na nikafikiria na kufikia ukweli muhimu sana, uliokusanywa na ndoto ile, nao ni:

 Hakika kuna maneno mawili, nayo ni mwanzo wa mambo yote ambayo yaliyowasibu wanadamu katika maisha yao ya kijamii, kutokana na kuporomoka katika tabia na maadili, nayo ndiyo chimbuko la migongano yote na hofu.

Hakika tumeyabainisha na kuyathibitisha katika (Neno la ishirini na tano), wakati wa kupima kwetu kati ya maendeleo ya kisasa, na hukumu za Qur’an tukufu, na hayo maneno mawili ni:

Neno la kwanza: (Nikishiba basi si juu yangu kufa mwenzangu kutokana na njaa).

Neno la pili: (Chuma wewe ili nile mimi, na taabika wewe ili nistarehe mimi).

Na jambo linalodumisha maneno haya mawili na kuyalisha ni: kuendelea riba, na kutotekeleza zaka.

Na hakika suluhisho pekee, na dawa yenye kunufaisha kwa ajili ya maradhi haya ya jamii ni: kutekeleza zaka katika jamii na kuifaradhisha kwa wote, na kuiharamisha riba kabisa, kwa sababu umuhimu wa zaka hautosheki kwa watu na jamii maalumu tu, bali ni nguzo muhimu katika kujenga furaha ya maisha ya ubinaadamu, na mahitaji yake yote ya maisha, bali ni nguzo ya kina ambayo inaimarisha kudumu maisha ya kweli kwa binadamu, hivyo kwa sababu ubinadamu una tabaka mbili: tabaka la watu maalumu, na tabaka la watu wote.

Na zaka inadhamini rehema na wema kutoka kwa watu maalumu kwenda kwa watu wote, na kuhakikisha heshima na utiifu kutoka kwa watu wote kwenda kwa watu maalumu.

Laa sivyo zitazidi dhulma na ukandamizaji kutoka kwa watu maalumu kwenda kwa watu wote, na kuchimbuka chuki na maasi ambayo huzidi katika vifua vya watu wa hali ya chini kwa matajiri.

Na kuendelea tabaka hizi mbili za watu katika mapambano maanawi yenye kudumu, na kuingia katika misukosuko ya tofauti zenye kupingana, mpaka kufikia jambo kidogo kidogo katika kuanza mapigano ya kivitendo, na kukabiliana juu ya kazi na rasilimali kama ilivyotokea Urusi.

Enyi waheshimiwa na wenye ufahamu mzuri wa ndani, na enyi watu wenye ukarimu, na wema! ikiwa hamjakusudia kwa wema mnaoutoa, kwa nia ya zaka, na ikiwa hamjafanya kwa jina la zaka, basi hakika jambo hilo lina madhara matatu, bali linaweza kuondoka bure bila manufaa, hivyo ni kwa sababu ikiwa hamjatoa na kufanya wema katika njia ya Allah (s.w), na kwa jina la Allah (s.w), hakika bila shaka mtatoa neema kwa kupata fadhila – maana yake – mtamfanya fukara, masikini chini ya furaha ya neema, na kumfunga minyororo yake, halafu mnakuwa ni wenye kuzuiliwa kutokana na kukubaliwa maombi yake ya kweli, kwa kuwa mnakuwa ni wenye kupinga neema pindi mdhanipo kwamba nyinyi ndiyo wenye mali.

Na ukweli nyinyi si lolote isipokuwa wasimamizi, mmeamrishwa munazisambaza mali za Allah (s.w) kwa waja wake, lakini mtakapotekeleza wema katika njia ya Allah (s.w) kwa jina la zaka, hakika mtapata thawabu adhimu, na kuchuma ujira mkubwa, kwa sababu mmeitekeleza katika njia ya Allah (s.w).

Na nyinyi kwa amali hii (kufanya hivi) mnadhihirisha shukrani kwa ajili ya neema ambazo amezitoa Allah (s.w) juu yenu.

Basi mtapata dua yenye kukubaliwa kutoka kwa huyo muhitaji, ambapo hakulazimika kujipendekeza na kukuogopeni, na akahifadhi heshima yake na hadhi yake, basi inakuwa dua yake safi.

Naam, pale itolewapo mali kwa kiwango cha zaka bali zaidi yake, na kutekeleza mambo mema kwa sura zake tofauti, na kutoa sadaka pamoja na kuchuma madhara makubwa mfano wa ria, na umaarufu pamoja na kusimbulia na kudhalilisha, kutokana na kutekeleza zaka, na kusimamia mambo hayo mema kwa nia yake, kwa ajili ya dini ya Allah (s.w), na kuchuma fadhila ya kufanya faradhi katika faradhi za Allah (s.w), na kuchuma thawabu kutoka kwa Allah (s.w), na kusifika na ikh-lasi na dua yenye kujibiwa. Alaa! Kumbe kuna tofauti kubwa kati ya watoaji wawili.

سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إلَّا مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ أَنْتَ الْعَلِيْمُ الْحَكِيْمُ

اللهُمَّ صَلِّ عَلَى سَيِّدِنَا مُحَمَّدٍ الَّذِي قَالَ: (الْمُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِ كَالبُنْيَانِ يَشُدُّ بَعْضُهُ بَعْضًا)

Ewe Allah! Mpe rehema na amani bwana wetu Muhammad ambaye amesema: (Muumini kwa muumini ni kama jengo moja linaloshikamana lenyewe kwa lenyewe).

وَقَالَ:(الْقَنَاعَةُ كَنْزٌ لَا يَفْنَى) At-tabraani, Al-muujamul Ausat 7/84; Al-baihaqi, Al-zuhd 2/88.

Na amesema Mtume (s.a.w): (Kanaa ni hazina isiyoisha)

 وَعَلى آلِهِ وَصَحْبِهِ أَجْمَعِيْنَ.. آمِيْن وَالْحَمْدُ للهِ رَبِّ الْعَالَمِيْنَ

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.