Malipo Ya Haraka Ya Mema Na Mabaya

Nukta ya kwanza

Hakika katika ukamilifu wa ukarimu wa Allah (s.w), na ukunjufu wa rehema zake, na uselelevu wa uadilifu wake, ni kuwa ameingiza thawabu miongoni mwa amali za wema, na kuficha adhabu ya haraka katika matendo ya uharibifu na maovu.

Hakika ameingiza ndani ya mema, mambo ya ladha ya kimoyoni kimaanawi kwa anavyokumbusha neema za akhera na kuingiza ndani ya maovu adhabu za kimaanawi kwa vinavyofanya kuhisi adhabu ya akhera iumizayo.

Kwa mfano: Kueneza mapenzi na amani katika safu za waumini, hakika ni hisani njema kwa muumini, na pamoja na jema hili ana ladha ya kimaanawi na kionjo cha moyoni na ukunjufu wa kimoyo katika hali ambayo inakumbusha thawabu ya akhera ya kimaada. Na mtu ambaye anakagua moyo wake anahisi kionjo hiki.

Na kwa mfano: Kueneza uhasama na uadui baina ya waumini, hakika jambo hilo ni ovu baya kabisa. Ovu hili linaingia katika adhabu ya kimoyo na adhabu iliyoje! Kwani inashika kuikaba moyo na roho kwa pamoja basi kwa kila anayemiliki roho yenye kuhisi na hima ya juu anahisi adhabu hii.

Mimi mwenyewe nilipita – uhai wangu wote – katika zaidi ya majaribio mia moja ya aina hii ya maovu. Nilikuwa kila ninapofanya uadui kwa ndugu yangu muumini naonja adhabu ya uadui huo. Hata haikubakia kwangu shaka kwamba adhabu hii hakika ni adhabu ya haraka kwa kosa langu ambalo nililolifanya basi ninaadhibiwa juu yake na kuhukumiwa kwalo.

Na kwa mfano: Hakika kuwaheshimu wenye kustahiki heshima na kudhihirisha upole na huruma kwa wenye kustahiki ni amali njema na jambo jema kwa muumini. Basi katika jema hili inapatikana ladha kubwa na starehe ya kimoyo kwa kiasi humpeleka mwenye kuwa nayo kujitolea muhanga maisha yake. Ukitaka tazama ladha waipatayo wazazi katika kutoa huruma zao kwa watoto wao, hata mzazi hupita kwa ajili ya huruma hiyo katika kutaabisha nafsi yake. Bali utaona hakika hii ni wazi hata katika ulimwengu wa wanyama, kuku humshambulia simba kwa ajili ya kulinda vifaranga vyake.

Kwa hiyo katika heshima na huruma kuna malipo ya haraka. Wale ambao wanaomiliki roho za juu na nafsi hodari za kishujaa wanaihisi ladha hiyo.

Na kwa mfano hakika katika pupa na israfu kuna adhabu ya kimaanawi ya haraka na malipo ya kimoyo, kwani humfanya mtu mwenye tabia hiyo mnyonge kutokana na wingi wa malalamiko na wasiwasi, basi utaiona adhabu kama hiyo bali zaidi kuliko hiyo katika hasadi na ushindani na wivu, hata hasadi humuunguza mwenye nayo kabla ya mwingine. Aya inageuka katika kutegemea na kukinai kwani katika mawili hayo kuna thawabu na thawabu iliyoje! Kwa namna ya kwamba inaondosha athari za misiba na hali za shida na uhitaji.

Na kwa mfano ghururi na kiburi ni mzigo mkubwa wa kuudhi unaomuelemea mwanaadamu, kwani anateseka kwa kuona kwake watu wengine wanavyoona uzito wake katika wakati ambao akisubiri wao kumuheshimu.

Naam, hakika heshima na utiifu hupewa wala havitafutwi.

Na kwa mfano: Hakika katika unyenyekevu na kuacha ghururi na kiburi kuna ladha ya haraka na malipo ya sasa hivi humkomboa mnyenyekevu kutokana na mzigo mzito nayo ni kujifanyisha na kujionesha. (Ria)

Na kwa mfano: Hakika katika dhana mbaya na tafsiri mbaya kuna malipo ya haraka katika dunia hii, mpaka ikawa “mwenye kugonga hugongwa” ni kanuni maarufu. Yule anayewadhania vibaya watu kwa vyovyote atafikwa na dhana zao mbaya. Na ambaye hufasiri matendo ya ndugu zake waumini tafsiri mbaya hapana namna atapata malipo hayo hayo hivi karibuni.

Na kama hivi, pima kwa mwendo huu matendo yote mazuri na mabaya.

Tunamuomba Allah (s.w) mwenye kurehemu awaruzuku wale ambao wanaonja ladha ya hali ya kimiujiza wa Qur’an wa kimaanawi unaotokana na Risale-i nur katika nyakati zetu hizi vionjo vya ladha hizo za kimaanawi zilizotajwa, kwa idhini ya Allah (s.w) zisiwakaribie tabia mbaya.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.