Nyongeza Ya Neno La Ishirini Na Sita Njia Ya Karibu Zaidi Kuelekea Kwa Allah

Nyongeza hii fupi sana ina umuhimu mkubwa na manufaa kwa kila mmoja.

Ili kuwa karibu na Allah (s.w) kuna njia nyingi, na kisima cha njia zote za kweli na sahihi ni Qur’an, ila baadhi ya njia zipo karibu zaidi kuliko nyingine na ni salama, pia ni za ujumla.

Nimefaidika na utukufu wa Qur’an, licha ya uchache wangu wa fahamu, kwamba njia fupi na sahihi ni njia ya ajizi, na ufukara na huruma na tafakuri.

Naam ajizi ni mfano wa mapenzi makubwa ni njia yakufikia kwa Allah (s.w), bali ni njia ya karibu na iliyo salama, kwani inafikisha kwa anayependwa kwa njia ya Al-ubudiyah, na mfano kama huo ni ufukara ambao unamfikisha mja kwa jina la Allah la.

“الرَّحْمَنُ “

Na pia huruma ni mfano wa mapenzi ni yenye kumfikisha kwa Allah (s.w), ila ni pana zaidi na inamfikisha mja katika jina la Allah (s.w) la,

“الرَّحِيْمُ”

pia tafakuri (akili) ni njia sawa na mapenzi bali ni kubwa zaidi na yenye muangaza, kwani tafakuri inampeleka mja kwa jina la Allah (s.w) la.

“الحَكِيْمُ”

Lakini isije kukupelekeni akili zenu kufahamu kinyume na makusudio, ama makusudio ya ajizi na ufukara na mapungufu, ni kudhihirisha haya mbele ya Allah (s.w) wala sio mbele za watu.

Nyiradi za njia hii fupi ni kukamatana na sunna za Mtume (s.a.w), na kutekeleza faradhi, hasa hasa kusimamisha sala kwa mujibu wa nguzo zake, kuleta adh-kar baada ya sala, pamoja na kuacha kufanya madhambi makubwa.

Chemchemi ya haya yote ni Qur’ani tukufu anasema Allah (s.w):

فَلَا تُزَكُّوا أَنْفُسَكُمْ Qur’an, 53:32

Aya inaonyesha hatua ya kwanza.

وَلَا تَكُونُوا كالَّذِيْنَ نَسُوا اللهَ فَأَنْسَاهُمْ أَنْفُسَهُمْ Qur’an, 59:19

Aya inaonyesha hatua ya pili.

مَا أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍ فَمِنَ اللهِ وَمَا أَصَابَكَ مِنْ سَيِّئَةٍ فَمِنْ نَفْسِكَ Qur’an, 4:79

Aya inaonyesha hatua ya tatu.

كُلُّ شَيْئٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ Qur’an, 28:88

Aya inaonyesha hatua ya nne.

Hatua hizi nne tunazisherehesha kwa ufupi:

Hatua ya mwanzo:

Kama inavyoelekeza aya tukufu

فَلَا تُزَكُّوا أَنْفُسَكُمْ

hili ni katazo kwa mtu kutakasa nafsi, kwani mwanaadamu kutokana na maumbile na fitra yake, ni mwenye kuipendelea nafsi yake, na daima anapenda na kuitanguliza nafsi kwenye kila kitu, anatolea muhanga kila kitu kwa ajili yake, na anapenda kujisifu sifa ambazo hastahiki isipokuwa Allah (s.w) muabudiwa, na anaitakasa nafsi yake, bali hakubali upungufu wowote katika nafsi yake na anailinda kwa nguvu kana kwamba ni ulinzi wa ibada, hadi kufikia sawa na mwenye kutumia zana alizopewa na Allah (s.w) za kumshukuru na kumtukuza kwa ajili ya nafsi yake, na hapo ndipo anapoingia kwenye aya:

مَنِ اتَّخَذَ إِلهَهُ هَوَاهُ Qur’an, 25:43

na huanza kushangazwa na nafsi yake na anaifanyia fakhari, hivyo ni lazima kuitakasa nafsi, na kuitakasa nafsi katika hatua hii ni kuitoharisha kwa kutoitukuza na kujitakasa binafsi.

Hatua ya pili:

Kama inavyotoa somo aya tukufu

وَلَا تَكُونُوا كالَّذِيْنَ نَسُوا اللهَ فَأَنْسَاهُمْ أَنْفُسَهُم

hakika mwanaadamu ni mwenye kuisahau nafsi yake na kughafilika, anapofikiria mauti huyaelekeza kwa mwingine, na anapoona kuondoka na kumalizika huelekeza kwa wengine, kama vile halimuhusu, kwani hakika nafsi inayoamrisha maovu ni yenye kujikumbuka katika sehemu ya kuchukua ujira  na hadhi zake, hivyo inakamatana nayo kwa nguvu, wakati huo huo inajisahaulisha sehemu ya amali na huduma na taklufa, hivyo kuitakasa nafsi na kuitoharisha na kuilea katika hatua hii ni kufanya amali kinyume na hali hii, yaani kutosahau katika kusahau kwenyewe yaani kuisahau nafsi katika hadhi na ujira, na kuanza kuifikiria katika kuhudumikia huduma njema na kufikiria mauti.

Hatua ya tatu:

Ni ile ambayo aya tukufu inaelekeza: ”

مَا أَصَابَكَ مِنْ حَسَنَةٍ فَمِنَ اللهِ وَمَا أَصَابَكَ مِنْ سَيِّئَةٍ فَمِنْ نَفْسِكَ Qur’an, 25:43

Inamaanisha kwamba nafsi daima ni yenye kupenda kujinasibisha na kila la kheri, hali inayoifanya iwe yenye kujifakharisha na kujistaajabisha. Mtu anatakiwa asiiyone nafsi yake ila ni yenye mapungufu, ajizi na ufakiri na aone yote mazuri na yenye ukamilifu ni ihsani tu ya Allah (s.w) kwake, na ayapokee kuwa ni neema za Allah (s.w) kwake, hivyo ashukuru badala ya kujifakharisha na badala ya kujidai na kujisifia, ama kujitakasa katika daraja hii kumo kwenye siri ya aya

قَدْ أَفْلَحَ مَنْ زَكَّاهَا Qur’an, 91:9

nayo ni kutambua kuwa ukamilifu wake umo kwenye kutokukamilika kwake, na uwezo wake katika ajizi yake, na ukwasi wake katika ufukara wake, (yaani ukamilifu wa nafsi ni kufahamu kutokamilika kwake, na uwezo wake upo katika ajizi yake mbele ya Allah (s.w), na ukwasi wake ni katika ufukara wake mbele ya Allah (s.w).

Hatua ya nne:

Ni ile ambayo aya inatafunza

كُلُّ شَيْئٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

hiyo ni kwa kuwa nafsi daima inajifanya kuwa iko huru inajitosheleza, hivyo hujidai aina ya ubwana, na kudhamiria uasi mbele ya Mola wake wa kweli, kwa kutambua ukweli huu ufuatao ndiyo mwanaadamu ataokoka na hilo, nao ni kwamba kila kitu kwa dhati yake na kwa maana yake ya kijina: Chenye kuondoka, chenye kupotea, chenye kuzuka na kutoweka, ila katika maana yake ya kiherufi na katika upande wa kutekeleza wadhifa wa kioo chenye kuakisi majina ya mtengenezaji mtukufu, na kwa kuzingatia wadhifa na kazi zake: Ni shahidi, mwenye kushuhudiwa, nae yupo na mwenye kupatikana.

Ama kuitakasa nafsi katika hatua hii ni kujua kwamba kutokuwepo kwake ni katika kutowepo, na kutowepo kwake ni katika kuwepo kwake, kwa maana ikijiona yenyewe ni yenyewe tu (kujitukuza) na ikadhani kuwepo kwake ndiyo kuwepo, hapo itatumbukia kwenye kiza cha kutengwa kupotea kusiko na kinachotosheleza kuingia viumbe vyote, kwa maana nafsi ikighafilika na uwepo wa uhakika wa Allah (s.w) na ikaghururishwa na kuwepo kwake yenyewe, itajikuta na upweke, inazama katika kiza cha kutengwa na kutokuwepo kwa kudumu, lakini nafsi inapoacha ubinafsi na  ghururi, na kujiona kwamba sio chochote bali ni sawa na kioo kinachoakisi, bali kuwepo kwake kunarudia kwenye kuwepo viumbe vyengine vyote.

Hakika yule anayemkuta Allah (s.w) ndani ya nafsi yake atakuwa amepata kila kitu (kheri), na viumbe vyote ni vyenye kutokana na majina yake Allah matukufu.You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.