MWALE WA PILI

بِسْمِ اللّٰهِ الرَّحْمٰنِ الرَّحِيمِ

اِذْ نَادَى رَبَّهُ اَنِّى مَسَّنِىَ الضُّرُّ وَاَنْتَ اَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ {Qur’an 21:83}

Dua ya Nabii Ayubu (as), bingwa wa subira, imejaribiwa vyema na yenye kufanya kazi, kukaribia kwenye aya, tunalazimika kutamka katika dua zetu,

رَبِّ اِنِّى مَسَّنِىَ الضُّرُّ وَاَنْتَ اَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ

Maana hasa ya kisa maarufu cha Nabii Ayubu (as), ni kama ifuatavyo:

Wakati ameathirika na majeraha mengi na vipele kwa muda mrefu alikumbuka jazaa kubwa inayoweza kupatikana kutokana na maradhi yake na aliyahimili kwa subira ya hali ya juu sana, lakini baadae wakati funza waliozalishwa na majeraha yake walipenya kwenye moyo wake na ulimi wake kiti cha dhikri na kumjua Allah (sw). Aliogopa kwamba jukumu lake la ibada litatatizika kwa hiyo alisema kwenye dua, sio kwa ajili ya raha yake mwenyewe, bali ni kwa ajili ya ibada yake ya kumuabudu Allah (sw).

Ewe Mola” maradhi yamenikumba kukutaja wewe na kukuabudu wewe kutakuwa kugumu” Allah (sw) akaijibu hii dua ya dhati isiyo na matakwa binafsi pamoja na kuwa kupata majibu mazuri ya kimuijiza. Allah (sw) akamtunuku Nabii Ayubu (as), Afya njema kamili na kaonesha kwake aina zote za huruma mwale huu unajumuisha ndani yake nukta tano.

NUKTA YA KWANZA

Kulinganisha baina ya majeraha ya nje na maradhi ya Nabii Ayubu (as) na sisi, basi sisi tumesibika na maradhi ya ndani nafsini na nyoyoni, na laukama hali yetu ya ndani ifanywe kuwa ni ya nje, tungeonekana kuwa tuna majeraha na maradhi zaidi kuliko Nabii Ayubu (as), kwa sababu kwa kila dhambi iliyotendwa na kila shaka ambayo inayoingia kwenye ubongo wetu inasababisha majeraha kwenye moyo na roho zetu.

Majeraha ya Nabii Ayubu (as) yalikuwa na tabia ambayo inaweza kutishia maisha yake ya kidunia, lakini majeraha yetu ya ndani yanatishia maisha yetu yenye uhakika wa kudumu kwa muda wa maisha ya milele, tunahitaji dua ya Nabii Ayubu (as) mara elfu kadhaa zaidi kuliko alivyofanya yeye mwenyewe. Ni pale tu wakati funza walipotokea kwenye majeraha yake mpaka kupenya ndani ya moyo wake na ulimi, hivyo vilevile madhambi ambayo majeraha yake yanatusababishia mitihani na mashaka, bila shaka maradhi hayo ni tija ya majeraha hayo Allah (sw) atulinde ndani ya nyoyo zetu, ambazo ni kiti cha imani, mpaka isifike kujeruhiwa imani yetu, na kupenya kwenye furaha ya roho na ulimi, ulimi ambao ni mkalimani wa imani, majeraha hayo yanasababisha kuacha kutamka dhikri na kumataja Allah (sw) na kuipunguza imani mpaka kufikia hali ya kunyamaza au kukaa kimya kusiko na maana.

Dhambi inayoingia kwenye moyo inautia moyo weusi na giza hadi kuzima nuru ya imani, ndani ya kila dhambi kuna njia ya kuelekea kwenye ukafiri, kama dhambi hiyo haitafutwa upesi kwa kutafuta msamaha wa Allah (sw), itakuwa ni kutoka kuwa kama funza na kuwa kama nyoka anayegonga vikali moyoni.

Kwa mfano, mtu ambaye kwa siri anatenda dhambi ya aibu, ataogopa fedheha itakayo patikana kama wengine watajua hilo, kwa hiyo kutokana na uwepo wa malaika na viumbe wa kiroho itakuwa ni vigumu kwake kuwavumilia, na atatamani kukana jambo hilo, japo kwa nguvu ya ishara ndogo mno.

Vile vile kwa mtu ambaye anayetenda dhambi kubwa anavyostahiki adhabu ya Jahannam angetamani kutokuwepo kwa Jahannam kwa moyo wake wote, na wakati wowote asikiapo tishio la moto wa Jahannam atathubutu kuukanusha kwa nguvu ya ishara ndogo na shaka, mpaka atakapochukua kinga ya ngao ya kufanya toba na kutafuta msamaha.

Vivyo hivyo, mtu ambaye hatekelezi swala za faradhi na kutimiza wajibu wake wa ibada ataathirika kwa udhia, sawa na kama akiwa katika kupuuzia wajibu mdogo kwa mtawala mdogo, ndio maana upotovu wake katika kutimiza wajibu wake licha ya amri inayorejewa mara nyingi ya mtawala wa tangu na tangu, atamdhikisha sana, na kutokana na dhiki hiyo kwa njia kama hiyo, atatamani kusema nafsini mwake: “ laiti kama kusingekuwa na wajibu huo” na kwa upande mwingine kutatokea kutokana na matamanio haya matamanio ya kumkana Allah (sw) na kuweka uadui kwake, kama kuna baadhi ya shaka kuhusiana na uwepo wa Allah (sw) mtukufu itakuja kwenye moyo wake atavutiwa kuikumbatia shaka hiyo kama ushahidi wa kuhitimisha, lango pana kwa uharibifu huo litafunguliwa mbele yake, mkanushaji hajui kuwa japo ametolewa kwa kukanusha kutokana na tabu ndogo ya wajibu wa ibada amejifanyia mwenyewe na ukanushi kama huo kuwa ni shabaha ya mamilioni ya shida ambazo ni kukatisha zaidi na kana kwamba anakimbia kung’atwa na mbu akikaribisha kugongwa na nyoka.

Kuna mifano mingine mingi inayoweza kufahamika kwa kurejea na hii mifano mitano kwa hiyo maana ya

بَلْ رَانَ عَلَى قُلُوبِهِمْ{Qur’an 83:14}

NUKTA YA PILI

Kama ilivyokwisha elezwa kuhusiana na mpango mtukufu, ujulikanayo kama hatima (Qadar) katika neno la ishirini na sita, watu hawana haki ya kulalamika katika hali ya majanga na maradhi, ni kutokana na sababu zifuatazo.

Sababu ya kwanza:

Allah mtukufuametengeneza nguo ya mwili ambayo amemvika mwanadamu ni onesho la sanaa yake, amemfanya mwanadamu kuwa ni kielelezo cha nguo ya mwili anavyokata, kupunguza kubadidilisha na kugeuza hivyo huonesha bayana ya majina yake kadhaa, kwa kiasi jina mponyaji (Al-shafy) ni lazima maradhi yawepo, pia jina la mtowaji riziki linahitajia njaa iwepo na kadhalika,

مَالِكُ الْمُلْكِ يَتَصَرَّفُ فِى مُلْكِهِ كَيْفَ يَشَاءُ

Bwana wa ufalme wote anayo haki kwa ufalme wake kama atakavyo,

Sababu ya pili:

ni kwa kupitia majangana maradhi maisha ndipo yanapoboreshwa, yanapokamilishwa, yanapotiwa nguvu na kuendelezwa ama uhai ambao unakwenda kwa mwendo mmoja na kupita katika tandiko la raha, maisha ya namna hiyo ni karibu zaidi na hali ya kutokuwepo ambayo ni shari tupu kuliko hali ya kuwa karibu na kuwepo ambayo ndio kheri tupu.

Sababu ya tatu:

Maisha haya ya Duniani sichochote isipokuwa ni medani ya majaribio na mitihani, mji wa amali na mahali pa ibada, na sio mahali pa starehe na kutaladhadhi wala sio mahali pa kupokea malipo na kupata thawabu, na madamu Dunia ni mahali pa kazi na ibada basi maradhi na misiba ukitoa yale ya kidini, na kwa sharti la kusubiri juu yake yanakuwa ni yenye kuwiana kabisa na mali hiyo bali yanarandana kikamilifu na ibada hiyo, kwani huipa amali nguvu na kuimarisha ibada, hafai kulalamika kwa ajili yake, bali inapasa kujipamba na kumshukuru Allah (sw) kwayo kwani hayo maradhi na shida hugeuza kila saa moja ya uhai wa mwenye kusibiwa kuwa ni ibada ya siku kamili.

Ibada ina sehemu mbili, sehemu hasi na sehemu chanya, sehemu ya kwanza inajulikana kwa wote, na ama sehemu nyingine ni mabalaa, madhara na maradhi, humfanya aliyesibika ahisi kushindwa na kuwa kwake ni dhaifu na anajihami kwa mola wake mwingi wa rehema na anaelekea kwake na kujilinda kwake na kwa hili anatimiza ibada iliyotakata, ibada hii ni yenye kutakata safi haingii ndani yake riyaa kabisa, mwenye kusibiwa akajipamba na subira na akafikiria katika thawabu ya madhara yake mbele ya Allah (sw), na uzuri wa malipo yake kwake atamshukuru mola wake kwa hilo, hapo itakuwa imebadilika, jambo la saa moja katika saa za umri wake ni sawa na siku nzima iliyotumika ndani ya ibada, na kugeuka umri wake mfupi kuwa umri mrefu mno, kuna kadhia nyingi ambazo dakika moja tu itahesabika kuwa na malipo ya ibada ya siku nzima.

Mara moja nilidhikika sana kutokana na ugonjwa mmoja wa ajabu uliomsibu mtu mmoja miongoni mwa ndugu zangu wa Akhera, Muhajir Hafiz Ahmed yalimpata maradhi ya hatari yakapita moyoni mwangu yafuatayo: “mbashirie kheri! kwani kila dakika katika dakika za umri wake huhesabika kuwa na malipo ya ibada ya siku nzima”.Alikuwa katika kila hali ndani ya maradhi yake akiegemeza hali hiyo na subira pamoja na shukurani.

NUKTA YA TATU

Kama tulivyobainisha katika neno la kwanza au la pili, yeyote yule atakayefikiria maisha yake yaliyopita, basi bila shaka itampitia ndani ya moyo wake kama si kauli ya “ Ah ” au “ Oh ” yaani ima atajuta na kusikitika, au atamhimidi mola wake na kumshukuru, kinacholeta masikitiko na majuto hakika huwa ni kwa sababu ya maumivu ya kimaanawi yanayotokana na kutoweka kwa matamu yaliyopita na kutengana nayo kwani kuondoka kwa matamu na machungu, bali yawezekana ladha ya kutoweka matamu ikasababisha mabaya ya kudumu ya kuendelea kufikiria, hukamua mabaya hayo na kuleta majuto na masikitiko wakati ambapo matamu ya kimaanawi na ya kudumu itokanayo na kutoweka kwa machungu ya muda mfupi ambayo aliyapitia katika uhai wake uliopita, humfanya ulimi wake kuwa wenye kutaja “ Alhamdu na shukrani kwa Allah (sw), hii ni hali ya kimaumbile kwa kila mwandamu anaihisi, ikiwa mwenye kusibiwa akifikiri zaidi ya hivi kwa kile ambacho mola wake amemuwekezea katika thawabu nzuri na malipo mazuri ya Akhera, akazingatia katika kugeuka umri wake mfupi kwa sababu ya masaibu na kuwa umri mrefu, hapo hatakuwa mwenye kusibiwa kutokana na madhara yalomfika tu, bali atapanda hadi daraja ya kumshukuru Allah (sw), na kuridhia Qadar yake basi ulimi wake utatamka kwa kumhimidi bwana wake mlezi kwa kusema;

اَلْحَمْدُ لِلَّهِ عَلَى كُلِّ حِالٍ سِوَلْ كُفْرِ وَ الضَلاَلِ

Imekuwa ni methali kwa watu kuwa; urefu ulioje wa zama za mabalaa! naam, iko hivyo, lakini sio kwa maana ambayo ipo katika mazowea ya watu na dhana yao kwamba ni mrefu kutokana na yaliyomo miongoni mwa dhiki na maumivu, bali ni mrefu wenye kuongezeka kama umri mrefu kutokana na matokeo makubwa ya kimaisha.

NUKTA YA NNE

Kama ilivyokwisha elezwa ndani ya makamo ya awali katika neno la ishirini na moja kwamba uwezo wa mwanadamu wa kusubiri masaibu aliopewa na Allah (sw) unaendana sana na hali yoyote ya masaibu, haishauriwi kujenga woga usio na maana, lakini kutokana na wingi wa upotevu, mwanadamu hughafilika na zile fikra zake kuona maisha haya ya mpito kuwa kama maisha ya milele, hupelekea kudhoofika nguvu za subira yake na kuitawanya katika maumivu ya muda uliopita, na hofu za mustakbali, haimtoshi ile nguvu aliyomwekea Allah (sw), katika subira kuhimili balaa linalomshukia na kuthubutu, anaanza kueneza malalamiko kana kwamba anamlalamikia Allah (sw) kwa watu, akionesha uchache wa subira na kwisha kwake namna inayofanana na wazimu, ukiachilia mbali haijuzu kwake kuhuzunika huzuni yake kama hii kamwe, hiyo ni kuwa kila siku katika siku zilizopita kama zilipita na mabalaa  uzito wake na mashaka yake yameshaondoka na imeacha raha yake, na machungu na tabu zake zimeondoka na imeacha tamu yake, usumbufu na dhiki yake vimeondoka na yamethibiti malipo yake, hivyo haijuzu kuyalalamikia, bali yapasa kumshukuru Allah (sw) kwa shauku na pupa, haijuzu kuchukia msiba bali yapasa kufungia kamba za upendo, kwani umri wa mwanadamu ni wenye kutoweka ambao tayari umesha malizika utabadilika kuwa umri mzuri wa kudumu muda mrefu kwa kiasi kile anacho taabika na mtihani, basi ni katika wehu na uwendawazimu wazimu mwanadamu kuteketeza sehemu ya subira yake na kuitupa kwa dhana na kufikiria mabalaa ambayo tayari yamesha pita na mumivu ambayo yamesha geuza kisogo, ama masiku yajayo, kwa kuwa bado hayajaja, na hayajulikani yamefichikana, ni katika upumbavu kuyafikiria kuanzia sasa na kuhuzunika kutokana na yanayoweza kumsibu mwanadamu katika masiku hayo kati ya maradhi na balaa, ni kama ilivyokuwa ni upumbavu mtu kula mkate leo sana na kunywa maji mengi, kuwa haitawezekana kumsibu njaa na kiu kesho au kesho kutwa, kadhalika kuumia na kulalama kutokea sasa kwa sababu ya yanayoweza kumsibu kwa muda wa mustakabali yakiwemo maradhi na masaibu mbali mbali ambayo sasa yamo katika hukumu ya visivyo kuwepo, na kudhihirisha majonzi upande wa hayo pasina na kuwepo sababu na ulazima, bali ni upumbavu na wehu kwa kiwango cha kuondosha upole na huruma juu yake, zaidi ya kuwa amejidhulumu mwenyewe.

Na muhtasari:

Kama shukurani inavyozidishaneema basi kulalamika kuna zidisha msiba na kuondosha kuhurumiwa na kusikitikiwa mwenye msiba.

Mtu mwema alipatwa katika mji wa “Erzurum” na maradhi ya hatari sana, na hii ni katika mwaka wa mwanzo wa vita vikuu vya kwanza vya ulimwengu, nikaenda kumuangalia akanitolea malalamiko yake.

Sijaona ladha ya usingizi tangu siku mia moja .

Nilizingatia malalamiko yake haya ya maumivu lakini wakati huohuo moja kwa moja nikakumbuka, na nikasema ;

Ndugu yangu! hakika siku mia moja kwa kuwa zimesha pita hizo kwa sasa ni kama siku mia moja za kufurahisha kwako usizifikirie wala usilalamike kwa ajili yake, bali zitazame katika upande wa kuondoka na kutoweka kwake na umshukuru mola wako kwa hizo, ama siku zijazo kwa kuwa bado hazijafika bado, basi tegemea juu ya rehema ya bwana wako mlezi mwingi wa rehema mwenye kurehemu na tulia kwazo. Usilie kabla hujapigwa, na usihofu pasipokuwa na kitu. Wala kutokuwepo usikutunuku pambo la kuwepo. tumia fikrazako katika saa hii tu, kwani unachomiliki katika nguvu ya subira inatosha kuthubutu saa hii, wala yasiwe mfano wa yule kamanda mpumbavu ambaye ametawanya nguvu zake katika kituo kulia na kushoto katika wakati ambao kikosi cha kulia na kushoto viliungana kikosi cha kushoto kwake na kukipa msaada na wakati ambapo upande wa kulia hakujakaa kivita bado, na punde adui alipojua hili alielekeza nguvu ndogo upande wa katikati na kulimaliza jeshi lake, basi ewe ndugu yangu usiwe kama huyu, bali kusanya nguvu zako kwa saa hii tu, na tazama rehema ya Allah kunjufu, na zingatia thawabu za Akhera, na zingatia katika maradhi kubadili umri wako wa kutoweka uliomfupi kuwa ni umri mrefu wa kudumu, basi tanguliza shukrani nyingi yenye kufurahisha kwa Al-Qadiir Allah mtukufu muweza wa kila kitu badala ya malalamiko haya yenye uchungu”.

Yule mtu aliyebarikiwa alifurahi kutokana na maneno haya na nafsi yake ikakunjuka, hata akawa anasema: “Al hamdu lillah” maumivu yangu yamepungua sana.

NUKTA YA TANO

Nayo ina masuala matatu.

Suala la kwanza:

Hakika ya msiba ambaouna hesabiwa ni musiba kweli na ambao ni kweli unadhuru, ni ule ambao unaisibu dini, hapana budi kutafuta himaya kutoka kwa Allah (sw) na kujitupa mbele yake na kunyenyekea kwake kwa maombi bila kuacha. Ama masaibu ambayo hayagusi dini, hayo katika ukweli wa mambo sio masaibu, kwa sababu sehemu yake ni; ni tanbihi ya mwingi wa rehema (sw), kwa mja wake ili amuamshe kutokana na kughafilika kwake, kama tanbihi ya mchunga kwa mbuzi wake pale wanapokiuka machunga yao, anayatupia jiwe, na mbuzi kwa upande wao wanahisi kwamba mchungaji wao anawazindua kwa jiwe lile na anawatahadharisha jambo la hatari la kudhuru, wanarudi kwenye machunga yao kwa kuridhia na kwa utulivu na ndio kama hivi mabalaa yanayo onekana mengi yake ni tanbihi ya Mwenyezi Mungu yana uamsho wa mwingi wa rehema kwa mwanadamu.

Ama sehemu nyingine ya masaibu ni kafara ya madhambi .

Na sehemu nyingine ya masaibu ni tunu ya kimungu kwaajili ya kutuliza moyo na kuumiminia utulivu ndani yake, na hii ni kwa kuondoa ghafla inayomsibu mwanadamu na kumfanya ahisi kushindwa kwake na ufakiri wake uliopo ndani ya maumbile yake .

Ama msiba ambao humkuta mtu kwenye maradhi ni kama tulivyo eleza huko nyuma kwamba huo sio msiba wa ukweli, bali ni upole wa mwingi wa rehema kwa sababu huko ni kumtakasa mwanadamu mu asafike kutokana na madhambi, na kumuosha kutokana na taka za makosa, kama ilivyopatikana katika hadithi sahihi, “hakuna muislamu yeyote ambaye anasibiwa na udhia, isipokuwa Allah (sw) atampukutishia makosa yake kama yanavyopukutika majani ya mti”

Na kama hivi, bwana wetu Nabii Ayubu (as), katika maombi yake hakujiombea nafsi yake na kutuliza raha yake, bali aliomba kuondoshwa madhara kutoka kwa Mola wake pale maradhi yalipokuwa ni kizuwizi cha kumdhukuru Allah (sw), Kwa ulimi, na kikwazo cha kutafakari ufalme wa Allah (sw) kwa moyo, akaomba ponyo kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kiibada kwa usafi na ukamilifu.Inapasa kwetu vilevile tukusudie kwa maombi hayo mwanzo wa tunalokusudia, kupona kwa majeraha yetu ya kimaanawi, na vidonda vyetu vya kiroho, yatokanayo na kutenda madhambi, yatupasa kumuelekea Alllah (sw). Muweza wa kila kitu wakati maradhi ya kimaada yanapozuilia kufanya ibada zetu kikamilifu. Wakati huo tunyenyekee kwake kwa udhalili wote, na tumuombe bila kutokea upinzami au kushtakia, na kulalamika kwani madamu tumeridhia kwa ridhaa yote iliyoenea basi ni juu yetu kuridhia na kusalimu amri moja kwa moja kwa kile Alla (sw), anatutunuku kwa ulezi wake, ama malalamiko ambayo yanaashiria kupinga hukumu na Qadar yake na kuonesha miguna na masikitiko, hayo yana fanana zaidi na kukosoa Qadar ya Mwenyezi Mungu yenye uadilifu na kutuhumu rehema yake kunjufu, basi yule anayeikosoa Qadar itampiga mweleka, na anayeituhumu rehema atanyimwa rehema hiyo.Kwamba kama kuutumia mkono uliovunjika kwa ajili ya kulipiza kisasi huzidisha kuvunjika zaidi, basi mwenye kupata mtihani kukabili msiba wake kwa kulalamika na kukereka na kupinga na kusumbuka nafsi na kuongeza balaa.

Suala la Pili:

Kila ukiyakuza masaibu ya kimaada hukua, na kila unapo yadogesha huwa madogo, mathalani; kila mwanadamu anapopata majonzi kwa sababu ya yanayoonekana kwake usiku miongoni mwa dhana, hukuwa hayo kwenye mtazamo wake, wakati ambapo akiyapuuzia hupotea, na kila mwanadamu anapoingilia kwenye nyumba ya madondola hujma yao huongezeka na kama atawapuuza hutawanyika.

Na masaibu ya kiada ni kama hivyo, kila mwanadamu anapo yakuza na kuyapa umuhimu na kupata majonzi hupenya kupitia dirisha la mwili na kuingia moyoni na kutulia humo, na wakati huo hukua msiba wa kimaanawi moyoni na kuwa umejikita kwa hali ya kimaada kwa msiba huu wa pili huendelea na kurefuka, lakini muda ambao mwanadamu atakapoondosha hofu kwenye mashina yake kwa kuridhia Qudra ya Allah (sw) Na kwa kutegemea rehema zake, hupungua huo msiba wa kimaada kidogo kidogo na kuondoka, kama maiti ambao hufa na kukauka majani yake kwa sababu ya kukatwa mizizi yake, na siku moja na ilielezea ukweli huu kwa maneno yafuatayo :

Na kutokana na malalamiko kuna mtihani,

Acha ewe masikini na fanya tawakkuli,

Maombi yako yasalimishe kwa Allah (sw).

Hapo vyote vitakuwa ni vipawa,

Vyote ni usafi,

Je analalama ambaye anabeba mgongoni mwake milima yote mikubwa,

Aje kulalamika kwa punje ndogo ya mchanga ? Hakika malalamiko

Ni mtihani juu ya mtihani,

Na madhambi ndani ya madhambi na taabu Wewe unapo tabasamu usoni mwa balaa Shida zitageuka zinahepa na kuyayuka Chini ya jua la haki kuna punje za baridi, Tahamaki Dunia yako ni tabasamu,

Tabasamu kutoka kinywani mwake inamwagika chemchemu ya yakini,

Tabasamu ya furaha kwa kuchanua kwa yakini, Tabasamu ya tahayari kwa siri za yakini.

Naam..! hakika mwanadamu anapopunguza ukali wa hasimu yake anapomkabili kwa furaha na tabasamu, shari ya uadui hupungua na kuzimika moto wa uhasama, unaweza kugeuka kuwa ni urafiki na kusuluhiana (kupatana), na ndivyo ilivyo katika kukabiliana na balaa kwa kumtegemea Muweza wa kila jambo ataondosha athari yake.

Suala la Tatu:

Kwa kila zama kuna hekimayake, balaa limebadili umbo lake katika zama hizi za mghafala, balaa haliwi balaa kwa baadhi ya watu daima, bali ni hisani ya Mwenyezi mungu na huruma kutoka kwake Allah (sw), na anawaona wenye kupewa mitihani ya madhara wakati huu kuwa wamebahatika wenye heri kwa sharti isiwe imegusa dini yao, kwangu maradhi na balaaa hayaleti kinachoyafanya yawe madhara kwa maoni yangu hadi iwe nayachukia, wala hayanipi huruma na maumivu kuwaonea waliofikwa nayo, hivyo hajanijia kijana mgonjwa isipokuwa namuona mwenye kufungamana zaidi na dini kuliko wenzake mfano wake, na mwenye kuambatana zaidi na akhera kuliko wao, basi nafahamu kutokana na hivi kwamba kwa haki ya hawa sioni balaa, bali ni neema, katika neema zake Allah (sw) ambazo hazihesabiwi wala kudhibitika, kwani maradhi hayo umpa mwenye nayo manufaa mengi kwa upande wa uhai wake wa akhera na inakuwa kwake ni aina ya ibada pamoja na kuwa inagusa maisha yake ya Dunia yenye kutoweka kwa sehemu ya mashaka.

Naam, huwenda akashindwa kijana huyu kuhifadhi aliyokuwa nayo kutokana na maradhi yake katika kushikamana na amri za Allah (sw), katika hali ile anapokuwa na afya bali anaweza kupondokea katika usafihi wa kuyumba kwa vijana na mihemko yake na kwa usafihi ulioenea zama hizi.

Hitimisho

Hakika Allah (sw) ameweka kwa mwanadamu udhaifu usio na mipaka, na ufakiri usio na ukomo, kwa kudhihirisha uweza wake, zaidi ya hivyo, ili kudhihirisha ufundi wake usio na mipaka wa majina yake, amemuumba mwanadamu kama mashine mwenye kuweza kupokea aina mbali mbali za maumivu kadhalika aina mbali mbali za furaha. Allah (sw) amemtengeneza kwa sura ya mashine ya ajabu ambayo inakusanya maelfu ya zana na masanduku, na kila moja katika hizo kuna machungu yake na ladha zake na majukumu yake na thawabu zake na jazaa yake, kana kwamba majina ya Allah (sw), Yaliyodhihiri ulimwenguni ambayo ni mwanadamu mkubwa yanadhihiri mengi yake pia kwa huyu mwanadamu ambaye ni ulimwengu mdogo na kama ilivyo kwake kuna mambo yenye manufaa, kama siha, afya, na ladha, na kinamfanya kumsukuma kwenye kuleta shukrani na kuiendesha mashine hiyo kutenda majukumu yake kutokea pande mbalimbali, hata mwanadamu anakuwa kana kwamba ni mashine ya shukurani, kadhalika hali ilivyo katika masaibu na maradhi na maumivu na baki ya viathiri vyenye kuhemeza na kuhangaisha, huendesha masanduku mengine ya mashine hiyo kwenda kufanya kazi na kushughulika na kuchokoza kutoka katika maficho yake na kuchimbua hazina za kushindwa, udhoofu ufakiri vilivyomo katika kiini cha uwanadamu. Masaibu hayamtunuku mwanadamu kumkimbilia Muumba kwa ulimi mmoja tu, bali humfanya anamuelekea na kumuomba msaada kwa ulimi wa kila kiungo katika viungo vyake kana kwamba mwanadamu kwa viathiri na sababu hizo na vizuizi na vipingamizi anakuwa ni kalamu yenye kukusanya maelfu ya kalamu. Hivyo anaandika makadirio ya uhai wake katika ukurasa wa uhai wake au katika ubao wa kimfano, na kufuma ubao wa kupendeza wa majina ya Allah (sw) mazuri, anakuwa mfano wa kasida ilyohifadhika, na ubao wa ilani, kwa hiyo anatekeleza jukumu la kuumbwa kwake.

Mwisho.

You May Also Like

Leave a Reply

Your email address will not be published.