
BISMILLAHIRRAHMANIRRAHIIM
KWA YEYOTE ANAYEHUSIKA
Ninaandika kukujulisheni kuwa BAKWATA imeitathmini Anatolia Foundation ambayo ni asasi inayotekeleza kazi mbalimbali za kibinadamu nchini.
Anatolia Foundation imeidhinishwa na BAKWATA, na inafuata maadili ya Ahlussunna Wal-Jamaa. Asasi inaendesha programu mbalimbali za Daawah ndani ya Tanzania. Asasi hii ina makao yake makuu Uturuki. Asasi imekusanya mkusanyiko wa Risale-i Nur (Vitabu 14 tafsiri ya Qur’an) na vimekubalika na kusambazwa na Serikali ya Uturuki.
Mkusanyiko mzima umeundwa kwa nguzo za imani.
Kwa hiyo BAKWATA linaidhinisha msaada wowote unaoweza kuisaidia Anatolia kuendelea na Shughuli zake Tanzania. Allah (s.w) akulipeni malipo yake bora kabisa hapa Ulimwenguni na Akhera inshallah.
Tunathamini sana msaada wako.
Wako Mwaminifu.