
Kitabu hiki kinatoa faida nyingi kuthibitisha kuwa Allah (sw) yupo na ni Mmoja kwa kuchambua baadhi ya maneno na sehemu ya Quran inayosomwa kwa kawaida wakati wa swala na baada ya kumaliza Swala. Maneno hayo yakiwemo kalima ya Tawhiid, At- Tahiyyaatu na Surat Alfatihat ( Alhamdu)
kwa mfano Al-Rahman, jina la Allah sw. hupewa maana ya Ar-Razzaq. Allah( sw) anatayarisha riziki za wenye Uhai wote , na hasa wasiojiweza na hususan watoto wa viumbe wote hai. Anawaandalia kwa namna ya ajabu nayo ikiwa nje ya hiari na uwezo wao. Tazama chakula cha watoto wachanga wa wanadamu, simba , ndege, na wengine wote.
kitabu kinatoa majibu kuhusu misiba na majanga na mitihani kama haipingani na rehema za Allah (sw)? Utakaposoma utapata maelezo ya kukinaisha pamoja na kukujulisha kuwa Allah (sw) yupo na ni mmoja wa pekee kwa Hoja za Uhakika.